Karibu tena, mawana Caribongo 'darasa huru'
Katika Makala hii, tutaangazia jinsi unavyoweza kujua gharama za uingizaji wa magari ,na kiasi gani kitatumika katika usajili wa gari au magari hayo.
Kwanza, ifahamike kua; Gharama gari zinazoagizwa kutoka japan kupitia ma kampuni kama BEFORWARD, CARFROM JAPAN, SBT TANZANIA n.k ni bei kabla ya kodi wala usajili wa gari au magari hayo (price excluding tax and duties), kwaiyo kabla haujaagiza gari ni vyema ujue taratibu na gharama za zoezi zima la usajiliwa gari lako.
Sasa, swali ni kwamba utajuaje gharama hizo?
KWANZA: Unatakiwa ujue aina na specifications za gari, kwamfano;-
- Make ya gari mf: TOYOTA,NISSAN,AUDI, BMW N.K
- Model na body ya gari mf: SEDAN, SUV, HATCHBACK, PICKUP,VAN AU WAGON
- Year of manufacture (mwaka iliotengenezwa)
- Country of origin (Nchi Inayotokea ) Mf: JAPAN
- Fuel type (aina ya mafuta inayotumia) mf: PETROL
- Engine size (ukubwa wa injini) mf: 2500CC
Ukiisha fahamu maelezo yote ya gari lako, kama yalivyo orodheshwa hapo juu, sasa unaweza ku BOFYA HAPA>>> Kisha jaza taarifa za gari lako na kisha bofya kitufe kimeandikwa 'CALCULATE'.. Upate mchanganuo wa gharama na jumla ya gharama za uingizaji na usajili wa gari lako.

No comments:
Post a Comment