Darasa huru...: Tamko la serikali ya Tanzania

Tamko la serikali ya Tanzania

Kwa kuzingatia kanuni ya 46 ya sheria ya afya ya jamii ninaelekeza mambo yafuatayo:
  • Kwanza watanzania wasiokuwa na safari za lazima wanashauriwa kwa sasa kusitisha safari zao kwenye nchi zenye maambukizi
  • Taasisi zote zikiwemo shule, hoteli, maduka ya biashara, nyumba za kulala wageni, makanisa, misikiti, ofisi za umma na binafsi, vituo vya kutolea huduma za afya, taasisi za fedha, vyombo vya usafiri pamoja na maeneo ya mikusanyiko ya watu kama vile masoko, viwanja vya michezo na vituo vya abiria kuweka vifaa vya kunawia mikono kwa maji yanayotiririka na sabuni au maji yenye dawa kwa ajili ya kuhakikisha usafi wa mikono.
  • Kuweka maji yenye dawa ya chroline katika mageti ya kuingia katika hifadhi zote kwa ajili ya kusafisha mikono ya watalii na waongoza wageni.
  • Kuepuka kusalimiana kwa kushikana mikono
  • Kukumbatiana , kubusu, kuepuka kushika pua, mdomo na macho.
  • Hospitali zote nchini za serikali na zisizo za serikali kuweka zuio la idadi ya watu ambao wanakwenda kuwaona ndugu zao. Kwa maelekezo ya waziri ni kwamba wageni wa kumuona mgonjwa wasizidi wawili kwa siku kwa kila mgonjwa mmoja.
  • Wananchi wametakiwa kutoa taarifa kwa vituo vya afya iwapo watamuona na mtu mwenye dalili za ugonjwa wa Covid- 19.

No comments:

Post a Comment

caribongo

Tamko la serikali ya Tanzania